top of page

KUHUSU SISI

Chuo cha mafunzo kilianzishwa mwaka 2016. lengo ni kuwafikia wafugaji wadogowadogo, mashirika yasiyo ya kiserikali, Idara za serikali na kutoa mafunzo ya kuku kwa kina na kwa muda mfupi.

Chuo chetu kimekaa katika mazingira tulivu na mazuri, ili kuwawezesha watu wanaokuja kupata mafunzo kujifunza na kutengeneza urafiki. Tunajivunia kuwa sehemu ya mradi wa APMI, kufanya kazi na shirika la kuku ulimwenguni ili kuleta mabadiliko. Hadi sasa zaidi ya watu 1000 wamepita katika chuo chetu na wanatupatia mrejesho ulio bora kuhusiana na kozi zetu. Tunaendelea kutoa mafunzo haya kila mwaka, na hata kuongeza vituo vingine kulingana na uhitaji.

UNGANA NA TIMU KAZI YETU

Sheryl.jpg
Sheryl Bradnick
Training Manager
Sarah.jpg
Sarah B Ndimbo
Administrator 

Upendo wangu kwa watu , ndio unanifanya mimi kuwa meneja wa mafunzo, kazi iliyo bora duniani! kuwa na fursa ya kufanya kitu tofouti ni heshima kwangu. Ni zawadi na tunu kukutana na watu waliotoka katka mazingira tofauti na kujenga urafiki usio na mwisho.

Mimi kama mwanamke naipenda kazi yangu na ninacho kifanya kila siku, kwa sababu sio tu ni sehemu ya kazi bali ni sehemu ambayo naweza kuonana na watu mbalimbali ambao naweza kuwapa ujuzi na kuwakaribisha. kila ninapolifikilia hilo inakua rahisi kwangu kuamka asubuhi na mapema.

IMG_7515.jpg
Mayai Mdiba
Trainer
Dr Dulle.jpg
Dr Charles Dulle
Consultant Vet and Trainer

Ni shake yangu kubwa kuwa vitu ninavyovitoa kwa njia ya nathalia na hasa kwa vitendo ni vitu ambavyo vinaenda kuisaidia jamii yangu na kuifanya iwe jamii ya kujituma na kuondokana na kutokuelimika juu ya masuala ya kielimu. Pia ni sehemu yangu ya kujivunia kuwa karibu na watu wa jamii yangu.

Princess Lay.jpg
Princess Laya
Mascot

I love what I do...it gives me goosebumps and makes my feathers stand upright. Seeing chicks on a Monday grow into chickens on a Friday...Kluck, Kluck, Kluck!

bottom of page